Välj en sida

Imani ya Kiinjili 2

Karibu kusoma bure kitabu cha Imani ya Kiinjili 2 juu ya Roho Mtakatifu, Kanisa na Maisha ya Kikristo. Unaweza kupakua kitabu kwa mfumo wa e-kitabu (eBook) hapa chini.

Juu ya Kitabu

Kitabu kinazungumzia yaliyomo ya Ukiri wa imani, sehemu ya tatu. Kimepangwa kwa ajili ya kufafanua kazi ya Roho Mtakatifu katika Kanisa (Waamini) na katika maisha ya Mkristo binafsi. Kwa hiyo kila kichwa chake kinamtaja Roho Mtakatifu kwa habari fulani. Kuna mafundisho ya kiimani pamoja ya jinsi mafundisho hayo yanavyohusu maisha. Walengwa ni wakristo wanaopenda kujifunza juu ya imani yao na hasa kwa wanafunzi wa uinjilisti na uchungaji wanaopaswa kufahamu na kufundisha mambo haya. Kiswahili cha kitabu ni rahisi.  Kuna michoro inayojaribu kueleza maana ya mada. Pia kuna maswali ya kutafakari na kujadili. Karibu kuendelea kusoma zaidi juu ya kitabu hiki katika dibaji. Kitabu kimetolewa na KKKT-Dayosisi ya Iringa pamoja na chama cha Swedish Evangelical Mission.

Juu ya Mwandishi

Mwandishi ni mchungaji Stefan Holmström kutoka Sweden. Amekaa Tanzania miaka mingi na kufundisha theolojia. Mchungaji Burton Wikedzi amemsaidia kuandika kitabu hiki. Endelea kusoma juu ya mwandishi na msaidizi wake kwenye katika kitabu chenyewe.

Mapendekezo

Askofu Blaston Gavile, KKKT-DIRA anaandika pendekezo nyuma ya kitabu:

Kitabu kinajaribu kujibu maswali mengi kuhusu Roho Mtakatifu kutokana na Neno la Mungu. Kinafundisha juu ya maisha ya kiroho na changamoto za kanisa la leo, kwa mfano uamsho. Mwandishi ameishi na kuhudumu kama mchungaji na mwalimu katika mazingira ya Kiafrika kwa miaka zaidi ya 30.

Mchungaji Dkt. Anneth Munga KKKT-DKM anasema:

Anayetafuta kitabu kinachofafanua juu ya Roho Mtakatifu na kazi zake kwa urefu, kwa upana na kwa kina asome kitabu hiki.

English summary

The title is Evangelical Faith – the Holy Spirit, the Church and the Christian Life. In an easily understood swahili it covers many aspects of the Third Article of Faith from a Lutheran and Charismatic perspective. Addressing contemporary issues in a Tanzanian context the author tries to guide towards a sound and positive reception of the work of the Spirit. The author is a former Swedish Evangelical Mission missionary with many years of experience of an African and
Charismatic environment, writing in dialogue with local Church Leaders. It suits especially Evangelists and Pastors but also the interested lay person and should be useful in many countries in Sub-Saharan Africa. For more information please write to stef.holmstrom(@)gmail.com.

Kupakua e-kitabu

Imani ya Kiinjili 2 kinapatikana kama e-kitabu za aina mbili. Ukipakua, tafadhali umjulishe mwandishi kwa njia ya barua pepe (stef.holmstrom(@)gmail.com).

Ukitaka nakala kabisa ya kitabu, wasiliana na mwandishi kwa barua pepe.